Nour Swirki
Mwanahabari kutoka mji wa Gaza, Mama wa Alia na Jamal.
19th October 2023, 9:19 am
Kila asubuhi na amka, nikiangalia dari. Hii dari si la nyumba yangu na wala hizi madirisha, penye kiwanda cha dobi zimewekwa. Kwa upande wa kulia na kushoto mimi na familia yangu tumelala kwenye safu pamoja tukiwa tumekaribiana. Lakini ni nani hawa watu walioko na sisi? Ni kivipi dunia imetuleta pamoja na tunalala kwenye sehemu moja na hatujawahi juana hata kwa sekunde moja. Kila siku nikiamka na matumaini kuwa hii ni janga la usiku tu, kuwa nitafungua macho kwa chumba changu cha kulala na niite msichana wangu Alia, anichemshie maziwa nitengeneze Nescafe na nikunywe karibu na mimea yangu, yenye imeweza kufa kwa sasa, kwa imeachwa nyumbani peke. Kila Asubuhi nafikiria kila taarifa ya habari na wapendwa wetu waliofariki tutawaona tena wakitungoja. Kila asubuhi, Mungu wangu, nahakikishani siku gani na tarehe gani…… muda umesimama ndani yangu kutoka asubuhi wa tarehe saba mwezi wa kumi (7th October) na sitaki muda ukipita baada ya hiyo siku. Kila asubuhi, Mungu Wangu, Lango la kuzimu hujifungua ndani yangu…. Mungu Wangu moyo wangu unauma.
20th October 2023, 9:06 am
Habari za asubuhi, wewe sayari mbaya ni siku ya kumi na tano leo. Mgongo wangu haujaacha kuniuma tokea jana………. Nalalia godoro moja na mwana wangu bila mto, na pia blanketi moja na wengine wawili. Na ndivyo kila mama anavyo fanya hapa. Inahisi kama anasa baada ya kulala kwenye shule tulichukua makazi…..kwenye sakafu chafu yenye iko na kila aina ya magonjwa duniani. Watu wakinikanyaga wakipita na naangalia miguu na kusikia wengine wakiomba msamaha na wengine kutojali mwili wangu uliojilaza sakafuni, kutopatia umuhimu wowote….
Siku yetu huanza saa kumi na mbili asubuhi, kwa sababu mpaka jana, kumekuwa na watoto watatu, mdogo akiwa mtoto wa wiki tatu anayeitwa Salem, mtoto wa kike anayeitwa Karmel, mwenye akona miezi isiozidi mbili na Kareem mwenye ako na miezi sita. Leo asubuhi, Mungu ametubariki na mtoto mchanga, mwenye atakuwa mwana wa kila mama mwenye amechukua makazi hapa, na jina yake ni Nidal……tunajaribu kutengeneza mahali ya nafasi ya kibinafsi ya mama na mwanawe tukingoja wafike chini ya moto mkali na uvamizi wa anga.
25th October 2023, 9:05 am
Nakosa nyumba yangu sana sana.
29th October 2023, 9:19 am
Baada ya mwasiliano kukatwa……tunashukuru Mungu tuko wazima, tuko hai…….jana muda ulirudi nyuma na ni siku ya kwanza ya majira ya baridi.
Tungekosa masaa nne ya kazi na watoto wangechangayikiwa na ratiba ya shule, lakini hayo yote hayakutendeka……….tumekosa muda wote wa maisha katika siku ishirini na moja. Israel hawajaweka muda nyuma ya dakika sitini.
Imewekwa nyuma nusu muongo. Imeangamiza nchi yetu tunayoipenda. Wakaua wapendwa wetu, wakatutenga kutoka dunia nzima, chini ya moto na mabomu makali jana. Angalau watu mia tano (500) waliuliwa.
1st November 2023,10:09 pm
Leo Alia ananiambia, “Mama, kuna uwezekano wa nyumba yetu bado kusimama?”
Ndio, kwa uwezo wa Mungu, tunakosa nyumba yetu. Tuko watano kama familia, Mama, Baba, mwana wa kike, mwana wa kiume na nyumba.
5th November 2023, 10:56 am
Kila wakati nikisoma kuhusu watu tunaowajua, waliofariki, kenye naona ni picha ya watu wanaoomboleza wapendwa wao, picha za maiti na watoto na uharibifu…. Nahisi kizunguzungu, kama ambaye naanguka kutoka gorofa milioni moja mpaka chini. Naanza kutoa jasho na kukosa pumzi.
Pengine hatuna wakati wa huzuni na hatuna wakati wa kulia, lakini mwili wetu unaitikia na mchanganyiko na njia ya kuchanganyikiwa…..
Bado tunajaribu kuishi na kupinga hasara wakati wa hali unaotisha, lakini mpaka lini tutavumilia?. Sijui, kwa uhakika sijui…..Ewe Mwokozi, tuokoe..
5th November 2023, 5:27
Ni wakati wa kawaida na natoka nyumbani kutoka kazini, nilikuwa naongea na fono kama kawaida salem ananipeleka nyumbani. Tukafika karibu mahali ya makazi yangu ninayoishi kwa muda kama mtu aliyehamishwa, ghafla barabara haionekani na kulikuwa na harufu ya unga wa bunduki…….nikaanza kumpigia salem kelele asiendelee kuendesha gari, wanaweza rusha bomu tena na kulikuwa na gari la wagonjwa nyuma yetu……..Salem ni mjasiri aliendelea kufuata gari la wagonjwa, akiniambia kuwa watoto wako kule na lazima tukawaone……. Sijui kama ilikuwa muda wa dakika mbili ama zaidi nikaona nyumba, “nikamwambia, ndio ile nyumba bado iko, ni sawa, ni sawa.”
Akanishukisha kwa gari yeye akaendelea kupeleka gari akifuata gari la wagonjwa…….nilivyohisi hizo dakika mbili ni kama maisha yangu yote. Nilivyohisi kwa mshipa na ufahamu. Nashukuru Mungu.
7th November 2023, 11: 25 am
Nakosa nyumba……nakosa Gaza… hakuna aliye bora kuliko mwengine……wapendwa na wasiojuana wanathibitiana kukuwa na subira……na wakati mwengine kwa maneno inayoleta mabadiliko wakati wa kukata tamaa…..kuendelea kujuliana hali…hali ya mazingira yetu yote imebadilika na natumai sisi hatutabadilika….Sisi wote tunaishi hali mbaya katika maisha zetu…… Sote tunajua ni wakati mgumu….mgumu sana….Ewe Mungu…. Tusikize!....
8th November 2023, 12:05pm
Tarehe nane mwezi wa kumi na moja mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu, saa sita na dakika tano mchana.
Mara ya kwanza kusafiri- nilikuwa mzee kama wengi wetu wagaza.,wenye wamenyimwa furaha- hoteli inanukia marashi ya peaches…..na tokea hiyo wakati, napaka nyumba yangu marashi ya peaches na kila nikifanya hivyo naambia Salem: “Mungu, kama harufu ile ya kusafiri.” Mpaka kila wakati nikipaka hiyo marashi nyumba: “unajua mama yako atasema nini? Harufu ya kusafiri” akinicheka….. mahali ya makazi ya wakimbizi, jinsi watu walivyo wengi tunatumia kisafishaji hewa yenye inanuka kama marashi ya peaches…..na kwanza hiyo wakati ikawa inanikumbusha masalani kwa wakimbizi…….
Vitu vidogo vilivyo tukumbusha wakati wa furaha, yote imeharibiwa sasa,…..pengine haya yanakaa kama mambo yasiyo na thamani kwa walioko nje wakisoma hii…….lakini moyo yetu huvinjika kutokana na haya mambo madogo.
11th November 2023, 8:25 pm
Leo sijafanya chochote, sijafanya kazi. Nimetoka nje kununua bidhaa kidogo ya kawaida……chakula na mbadala. Ilituchukua muda wa masaa moja kutembea na kuenda kwa duka tano kununua bidhaa zengine tunazo hitaji……maduka hayana bidhaa…..nilishinda hapa penye hata sijui niite vipi, lakini kwa uhakika sitaita “nyumba yangu” ama nyumbani….nyumba yangu na nyumbani ni huko Gaza……siku nzima nimeshikilia rununu yangu ya mkono kuangalia mapicha……saa zengine nacheka na saa zengine ni kama roho yangu inawaka moto……nimeshinda nikisema, Mungu, ingekuwa si hizi picha ningedhani kila kitu katika maisha yangu ni ndoto. Kama ambaye ni maisha ya nyumba isiokuwa na usahihi kuwa ilikuwepo…… napigia marafiki na tukitaniana……sote tuko na ufahamu kuwa haya ni mazito kuvumilia na sote tunataka kurudi…..nilikuwa nikiwauliza: “tutarudi kweli?” na sisi wote hatujui,na jibu nzuri ilikuwa “hadithi yetu ni mrefu, lakini tutarudi”……kitu ya wasiwasi kurudi ni kuona picha za wanajeshi na tanki kwenye mahali kama, Aljundi, Albahr, Alrimal, Alsin’a…….sijui hii vita itaisha lini na ni lini tutarudi!
Najua napenda nyumba yangu na napenda Gaza.
Nimesema hivi kwa muda mrefu na watu wananicheka. Kila nikisafiri na nirudi narudi na machozi kwa macho yangu kwa mpaka ya kuvuka, kwa sababu nimeikosa na wananiambia mimi nina wazimu, unapendea nini Gaza, hama….lakini naipenda sana, kiasi ya kuwa moyo wangu haiezi fahamu…..nahisi kama nakosa kitu kwa nafsi yangu.
Nakukosa, nyumba yangu, nakukosa Gaza.
(Nour, bwana yake na mwanawe walikimbia nyumbani kwao mji wa Gaza. Bado anaandika kutoka makazi anapoishi).