Ebraheem Matar
Daktari katika Sadaruki kwenye hospitali ya Al Aqsa Martyrs na mwanablogu kutoka Gaza
okt 11 2023
Shajara ya shahidi katika vita , kama daktari kwenye hospitali za Gaza
Ewe Mungu , nimeona kila kitu(vya ajabu) , nimeona watu wakikimbilia hospitalini baada ya kupigwa bomu wakiwa wamejawa na Damu , mchanga na jivu. Nimeona nyuso zao zikiwa zimejawa na mshtuko kutokamana na matukio wanayopitia na wakiwa katika hali wasiyojitambua. Nimeona mili yao ikiwacha kupumua kwasababu ya moshi ulioningia vinywani mwao ama pia kwasababu vyuma vilikata ngozi iliyoko vifuani mwao
Nimeona mili ikija na ikiwa imejawa na vumbi mithili ya sponji iliyotiwa vumbini. Nimeona watoto wakitokwa na damu na kupoteza fahamu katikia kipindi kirefu kwasababu mawe makubwa yaliwaangukia vichwani mwao. Niliona watu ambao tango zao , viungo vyao n majina yao yakibadilishwa kwa chanzo cha kuwa wakati mwengine ilikuwa vigumu kutambua mili. Wangesema “ safisha uso wake utoe vumbi, pengine tutamtambua” wangefanya hivyo ndiposa wangemtambua , mwanaume mpole na mkarimu , aliyekuwa ameketi nyumbani mwake, kwa sababu hakukuwa na na pahali pa kwenda
Nimeoma kina mama wakikimbi kwenye ukanda, wakilia kana kwamba imefika mwisho wa dunia mioyoni mwao , wakihema na kuuliza maswali chungu nzima huku wakipiga mayoe “ Je wako hai? Nani ako hai ? Watoto wangu wako wapi ? Ewe mungu , hao ndio niko nao peke yake”
Nimeona watu walioshtuka na kushangaa kwa sababu ya idadi kubwa ya walioathirika
“ ni idadi gani ya wafu tumehesabu leo ? Tulifanya makosa? Katika saa lililopita tulipokea watoto wawili waliofariki na watoto wawili waliokuwa wakitokwa na damu kwa wingi vichwani mwao. Barobaro kumi waliletwa hospitalini na mili yao haikuonesha kuwepo kwa ishara muhimu kama kiwango cha presha na upigaji wa damu mwilini (walikuwa wamefariki) hii ilifanyika kwa wakati mmoja, vipande vya nyama,viungo vya mwili vikiletwa kwenye vifuko vidogo huku vichwa vikumwagika maji ya ubongo”
Nimeskia sauti za waliofiwa wakipiga mayowe mpaka koo zao zikawauma na sauti zao zikipaa hewani, wakipiga kelele kwenye maskio ya wapendwa wao waliofariki wakiuliza:-
“Umeenda wapi ukaniwacha ? Nani atabaki na mimi baada yako wewe?
“Hukuniambia kwamba ungeondoka, unganiambia ili nikuage”
Niliskia mtu akisema “ Mungu sisi ni watu maskini wazuri mbona haya yanatufanyikia?”
Nimeona watu wakiongelelea habari, siasa na matokeo ya vita, wakitoa maoni, kisha wao wakageuka habari kwenye ripoti za habari. Nimeona wafanyikazi wenzangu na kuwasalimia asubuhi mara jioni kuwapa pole kwa kufiliwa na familia zao. Wengine nliokaa nao walishangaa na kuuliza “kwamba watu waliokuwa wamefariki walikuwa hai kama saa moja lililopita , walikuwa kama sisi, wakati wetu utafika saa ngapi?”
Okt 14 2023
Aina tofauti ya walioathirika na vita sembuse na wale walioumia
Leo , mwanamume mwenye umri wa maika sitini aliokuwa na ugonjwa wa moyo aliwasili hospitalini. Aliugua kutokamana na mashambulizi ya angina , yaliyofanya damu yake mwilini kushuka kwa hali ya juu, hili tendo likafanya moyo wake ukaacha kupiga
Je, hili tukio lilitendeka vipi?
Alipokuwa anahama na watoto wake wakiwa ndani ya gari , wakitoka Gaza wakielekea kusini. Alipoona makombora ya roketi ikitua kwenye vichwa vya waliotolewa makwao wakisafiri kwenye “Salah al Din Street”. Alijawa na hofu , mshtuko na dhiki , alihisi haya yote pamoja na huzuni aliyohisi kwa sababu ya yeye kuondoka nyumbani na mjini mwake kama mkimbizi
Kiukweli , kuna waathiriwa wa aina tofauti hapa, Kuna watu ambao hawajaathirika moja kwa moja , hawa ni watu amabo hushtuka kama binadamu yeyote. Kiwango cha uwoga na huzuni na kufa moyo iko juu sana. Inaweza kuwa sababu ya mioyo yao kuacha kupiga
Okt 14 2023
Kuhusu hisia za kuona jiji lako unalopenda likianguka, kuona mitaa unayopenda ikiharibiwa, maeneo unayopenda, na bahari unayoipenda, na kuona marafiki na wapendwa wako wakianguka mmoja baada ya mwingine, bila mtu yeyote kuwasaidia. Haya yote yanatosha kuumiza moyo wako, na kukufanya ufe ganzi kutokana na maumivu makali na mshangao. Ewe Mungu, tunapitia mengi sana
Ndoto yangu ilikuwa kuishi maisha ya kawaida Gaza, kama mtu yeyote ulimwenguni, anayeishi katika nchi ambayo alizaliwa. Nilifurahi nyumbani, kazini, kwenye mikahawa, na marafiki. Hiyo ilikuwa zaidi ya kutosha. Nilithamini sana ukaribu wangu na baba, mama, ndugu, miti, na bahari. Nilichukia wazo la kuhamishwa na sikutaka kulipitia. Ee Mungu, nilikosea sana?
Dec 24 2023
Najiuliza, je siku moja nitaponea na kurudi Gaza kipenzi changu? Je, nitarudi kufanya mambo rahisi ninayopenda?
Kuchukua matembezi marefu katika mitaa yake, tukikaa kando ya bahari asubuhi na mapema ili kutafakari bahari kubwa ya samawati na anga pana juu, tukijua kwamba anga na bahari ndio uhusiano wetu pekee na ulimwengu wa nje.
Je, nitarudi kusikiliza muziki kando ya bahari na marafiki, huku tukizungumza, tukicheka na kuudhihaki ulimwengu, tukiimba na kuzungumza hadi asubuhi?
Je, nitakaa tena katika mkahawa huo unaotoa kahawa hiyo ya ajabu na keki ya ajabu ya Nutella, na kujisikia kama niko katika jiji maridadi zaidi duniani? Je, nitarudi kukaa na mama yangu kando ya bahari kutazama machweo ya jua, kushuhudia na kusherehekea jua likiogelea baharini? Tukio ambalo mama yangu analipenda sana, na anafkiri ndilo tukio zuri zaidi maishani? Je, tutatembea usiku siku za baridi ili kuhisi upepo mwepesi ukituchoma mashavuni na kugusa matone ya mvua kwa mikono yetu?
Je, tutarudi kwa kutembea polepole chini ya kitongoji cha Al-Rimal na kuwa na wakati mzuri wa maisha yetu katika Soko la Omar Al-Mukhtar? Je, tutarudi kwenye chakula tunachopenda zaidi? Sandwichi ya falafel yenye mchuzi moto kutoka Al Soussi, ikifuatiwa slushi ya limau kutoka Kazim Ice Cream- mchanganyiko wa ladha zaidi duniani?
Je, tutasoma tena chuo kikuu, kisha tukae katika Hifadhi ya Al-Katiba?
Kuangalia kijani mkali wa nyasi, na kupumua katika hewa safi; kiyoyozi chetu cha asili kinachotoka kwenye miti na baharini, kama mjomba Abu Ahmad anavyosema, wakati akituandalia chai.
Je, wanaume watarejea kwenye bandari ya Gaza saa kumi na mbili asubuhi kununua samaki wabichi mara tu wanapotoka baharini? Ee Gaza, je, kwa mara nyingine tena tutakula samaki kutoka katika bahari yako, tujaze matumbo yetu bila kikomo, na tutalemewa na furaha?
Je, tutarudi tena kufanya ziara katika maji ya bahari kwenye mashua kutoka bandarini?
Je, familia hiyo nzuri, kuanzia babu hadi mtoto, itarudi kwenda baharini kwa basi kubwa Ijumaa asubuhi ili kukaa hadi usiku? huku watoto wakisherehekea na kuogelea mpaka roho zao ziguswe na chumvi na mchanga, wakicheza na kufurahi mpaka wakachoka?
Je, nitarudi kutembea asubuhi kando ya bahari bila kushikwa na kombora lolote?
Je, nitarejea kwenye ndoto ya kuwa bingwa wa mabingwa wote katika gym hiyo ya kifahari ninayoipenda, kisha niende kufanya manunuzi katika jumba la kifahari zaidi ulimwenguni- Carefour?
Je, nitarejea kwa kuzingatia kwamba Gaza inatosha kunitosha kutoka katika miji yote duniani, na kwamba sifa zake rahisi zina uwezo mkubwa wa kutoa maisha kamili? Je, nitarudi kuchukia kuhama ng’ambo, na kujaribu kukaa karibu na baba, mama, mti, na nyumbani?
Je, tutarudi katika kutembea barabarani bila kuogopa kujikwaa juu ya maiti barabarani, au mti uliovunjika, au jengo lililolala chini?
Je, tutajua kutembea barabarani na hata lami, badala ya mawe yaliyovunjika? Ee Mungu, tutaamka kutoka kwa jinamizi refu la vita na kurudi Gaza?